Winga wa Chelsea Hakim Ziyech hajajumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Morocco kitakachoingia kambani kujiandaa na mashindano ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika AFCON 2022 nchini Cameroon.
Nyota huyo wa zamani wa Ajax, mwenye umri wa miaka 28, alikosa mechi zote sita za kufuzu Kombe la Dunia 2022 Qatar, na mara ya mwisho kuichezea timu ya taifa ya Simba wa Milima ya Atlas ilikuwa dhidi ya Burkina Faso mwezi Julai.
Zinatajwa sababu nyingi za kuachwa kwake, lakini mgogoro wa chini chini ya fowadi huyo na kocha Vahid Halilhodozic kuwa ndiyo kikwanzo.
Morocco iko kundi C kwenye kundi lenye timu kama Ghana, comoros na Gabon, mechi ya Afcon 2022 zitaanza Januari 9 ambapo kikosi kizima cha Simba wa Milima ya Atlas hiki hapa;
Makipa: Yassine Bounou (Sevilla, Spain), Monir El Kajoui, (Hatayspor, Turkey), Anas Zniti (Raja Casablanca, Morocco).
Walinzi: Achraf Hakimi (Paris Saint-Germain, France), Sofiane Alakouch (Metz, France), Souffian El Karouani (NEC Nijmegen, Netherlands), Adam Masina (Watford, England), Sofian Chakla (OH Leuven, Belgium), Samy Mmaee (Ferencvaros, Hungary), Romain Saiss (Wolves, England), Nayef Aguerd (Rennes, France).
Viungo: Aymen Barkok (Eintracht Frankfurt, Germany), Sofyan Amrabat (Fiorentina, Italy), Faycal Fajr (Sivaspor, Turkey), Azzedine Ounahi (Angers, France), Ilias Chair (QPR, England), Imran Louza (Watford, England), Selim Amallah (Standard Liege, Belgium).
Washambuliaji: Munir El Haddadi (Sevilla, Spain), Zakaria Aboukhlal (AZ Alkmaar, Netherlands), Abdessamad Ezzalzouli (Barcelona, Spain), Sofiane Boufal (Angers, France), Ryan Mmaee (Ferencvaros, Hungary), Youssef En-Nesyri (Sevilla, Spain), Ayoub El Kaabi (Hatayspor, Turkey).