Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafungwa 100 wa vita kuachiliwa katika siku ya Eid al-Adha

Wafungwa 100 Wa Vita Kuachiliwa Katika Siku Ya Eid Al Adha Wafungwa 100 wa vita kuachiliwa katika siku ya Eid al-Adha

Wed, 28 Jun 2023 Chanzo: Bbc

RSF nchini Sudan imetangaza leo kuwa itawaachilia wafungwa 100 wa vita ikiwa ni sehemu ya sherehe za Siku kuu ya Eid, huku upande wa upinzani wa serikali ukitangaza kuwa hakutakuwa na mapigano leo.

Leo asubuhi Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan alitangaza likizo ya siku moja ya kusherehekea Eid al-Adha.

Hii ni moja ya siku muhimu zaidi katika kalenda ya Kiislamu ya ulimwengu.

Taarifa iliyotumwa kwenye akaunti ya Facebook ya serikali ya Sudan inasema kwamba "siku hii ya Eid, jeshi linatangaza kusitisha mapigano katika siku ya kwanza ya Eid al-Adha."

RSF mnamo Jumanne pia ilitangaza kwenye Facebook kwamba kutokana na likizo ya Eid al-Adha, itawaachilia wafungwa 100 wa vita siku ya Jumatano.

Taarifa ya RSF inasema kwamba walioachiliwa "walinaswa na mamlaka zao na kutumwa kupigana vita ambavyo havikuwa vyao".

Matangazo haya yanakuja huku kukiwa na ripoti za mapigano makali kati ya pande hizo mbili katika mji mkuu Khartoum - ambao umezingirwa kwa zaidi ya miezi miwili - na katika miji mingine kama vile Bahri, Omdurman, na kwingineko.

Wakati RSF ilikuwa imetangaza kusitisha mapigano kuanzia Jumatatu, mapigano yaliendelea katika maeneo mengine ya majimbo ya Kordofan Kaskazini na Blue Nile.

Zaidi ya watu milioni moja wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano yaliyozuka mwezi Aprili (4), huku kati ya 3,000 na 5,000 wamekufa, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Chanzo: Bbc
Related Articles: