Mamlaka ya afya nchini Sudan inasema watu kumi na saba wakiwemo watoto watano wameuawa katika shambulio la anga kusini mwa mji mkuu, Khartoum.
Jeshi la Sudan na vikosi vya upinzani Rapid Support Forces (RFS) wamekuwa wakipigania udhibiti wa nchi hiyo kwa wiki tisa.
Maafisa wanasema takriban watu elfu mbili wamekufa - na zaidi ya milioni mbili wamelazimika kuyahama makazi yao.
Jeshi la Sudan limeongeza mashambulizi yake ya anga huku likijaribu kuteka Khartoum.
Jenerali wa jeshi alikuwa ameonya watu kukaa mbali na Shambulizi la anga lasababisha vifo ikiwemo watoto Sudan yanayokaliwa na Vikosi vya Rapid Support Forces.
Lakini raia wako katika hali ngumu kwa sababu wapiganaji wa RSF wamejikita katika vitongoji vya mji mkuu.
Watu wamekwama kati ya vikosi vya upinzani.
Watoto ni miongoni mwa wahanga wa shambulizi hili la hivi punde la anga ambalo pia liliharibu takriban nyumba ishirini na tano katika eneo maskini lenye watu wengi jijini.
Katika mkoa wa magharibi wa Darfur wanamgambo wa Kiarabu wameendelea kushambulia raia na kulazimisha idadi kubwa kutoroka mpaka na kuingia Chad.
Jitihada mpya ya kukomesha vita hivi inahitajika sana.