Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliofariki kwa ajali ya Mafinga wafikia 20

Walifarikipic Ajali ya Mafinga

Fri, 10 Jun 2022 Chanzo: Tanzania

Idadi ya watu waliofariki kwenye ajali ya Costa kugongana na lori lililokuwa limeharibika karibu na eneo la Changarawe, Mafinga mkoani Iringa imefikia 20.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema chanzo cha ajali hiyo iliyotokea leo Ijumaa Juni 10, 2022 ni uzembe wa dereva wa gari hiyo iliyokuwa inatoka Dar es Salaam kwenda Mbeya.

Amesema awali, dereva wa costa alipoteza mwelekeo na kuligonga roli ambalo lilikuwa limepata ajali kwenye eneo hilo.

Ameeleza kuwa wakati abiria walionusurika wakiokoa majeruhi, lori jingine aina ya Volvo liliwagonga abiria waliokuwa wakiokolewa kwenye ajali ya kwanza na kusababisha vifo vingi zaidi.

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Saad Mtambule amesema hali za majeruhi zinaendelea vizuri na kwamba, wengine wamehamishiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa ajili ya matibabu zaidi.

Amewataka madereva kuwa makini wanapokuwa kwenye wilaya hiyo kutokana na hali ya ukungu hasa nyakati za jioni, usiku na asubuhi.

Chanzo: Tanzania
Related Articles: