Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi amzika mama yake kisha kwenda kufanya mitihani

Dfdfdf 860x484.jpeg Mwanafunzi amzika mama yake kisha kwenda kufanya mitihani

Mon, 1 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idadi ya watu waliofariki kwenye ajali ya gari ndogo aina ya Noah iliyosombwa na maji iliyoyokea katika kata ya Maluka Wilayani Arumeru Mkoani Arusha, imefikia watano.

Hii ni baada ya Angel Metili ambaye ni mama wa mwanafunzi Careen Metil huku ikimlazimu mwanafunzi huyo kuondoka kwenda kufanya mitihani ya kidato cha sita inayotarajia kufanyika Mei 2, 2023.

Careen amesema aliwazika ndugu zake wanne waliofariki ndani ya wiki moja na leo anaelekea shuleni kuelekea kufanya mitihani ya kidato cha sita.

“Namshukuru Mungu amenisaidia hadi hapa nilipofika na nina uhakika naenda kufanya mtihani na uhakika nitaenda kufanya mitihani vizuri, Mungu ndiye ananipa imani, taarifa za msiba wa mama niliambiwa na baba mkubwa wangu ni mipango ya Mungu," amesema Careen.

Ajali hiyo ilitokea wiki iliyopita baada ya gari walilokuwa wakisafiria kwena kwenye mahafali ya mwanafunzi huyo kusombwa na maji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: