Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zimamoto waokoa maisha ya dereva kwenye ajali

Ajali Strs Zimamoto waokoa maisha ya dereva

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtu Mmoja kati ya Wawili waliokuwa wamebanwa kwenye gari kufuatia ajali iliyotokea Usiku wa kuamkia leo eneo la Miono wilayani Chalinze mkoani Pwani ameokolewa akiwa hai.

Kamanda wa jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa Pwani Jenifa Shirima amesema Majeruhi huyo aliejulikana kwa majina Mbwana Said.

Umri 37 Kabila Mzigua na Dereva wa Gari T118CAR ameokolewa baada ya Askari wa kikosi cha zimamoto na Uokoaji kufika eneo la tukio huku wakitumia vifaa vya kisasa vilivyopo kwenye gari yao mpya walifanikiwa kutengeneza nafasi na kisha kumtoa akiwa hai na kukimbizwa Hospitali kwaajili ya kupatiwa matibabu.

Pia Jenifa Shirima amesema kuwa katika kuhakikisha kazi za uokoaji zinafanyika kwa ufanis tayari serikali imelipatia jeshi la zimamoto gari mbili mpya za kisasa zenye vifaa maalumu vya Uokoaji zinapotokea ajali barabarani.

Mkuu huyo wa zima moto ametoa wito unaowataka wananchi kuwa panapotokea ajali au matukio kama hayo kuwasiliana na jeshi la zimamoto haraka kwa namba 114 ili wawahi kuokoa Maisha na Mali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: