Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sita wafariki ajalini, wengine wanane wajeruhiwa Arusha

Ajali Arusha Daladala.jpeg Sita wafariki ajalini, wengine wanane wajeruhiwa Arusha

Fri, 15 Sep 2023 Chanzo: mwanachidigital

Watu sita wamefariki dunia na wengine wanane kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wamepanda kuacha njia yake na kwenda kugonga mti katika eneo la kisongo mkoani Arusha.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo, amesema ajali hiyo imetokea Majira ya saa 11:30 jioni ikihusisha gari ndogo 'daladala.'

"Waliofariki bado hawajatambulika majina ambapo wanaume ni wanne na wanawake ni wawili na bado chanzo halisi cha ajali hakijajulikana, hata hivyo; taarifa za awali zinaonyesha ni mwendo kasi" amesema Kamanda Masejo.

Amesema kuwa gari hilo la abiria lilikuwa linatokea Wilaya ya Karatu kuja Arusha, ambapo inadaiwa kuwa dereva alishindwa kuhimili gari alipotaka kuyapita magari mengine ndipo akaacha njia na kwenda kugonga mti.

"Miili imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospital ya Rufaa Mount Meru na Majeruhi wote tumewaleta hapa hapa hospitalini kwa ajili ya matibabu zaidi.

Kamanda Masejo amewataka wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi kutambua miili ya marehemu lakini pia ndugu zao ambao ni majeruhi.

Chanzo: mwanachidigital
Related Articles: