Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali Bagamoyo yaua bosi wa benki, mhadhiri wa Mzumbe

Ajali Bagamoyo Bagamoyo (600 X 313) Ajali Bagamoyo yaua Bosi wa benki, mhadhiri wa Mzumbe

Thu, 3 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ajali ya gari, iliyotokea jana Jumatano usiku katika kijiji cha Mapatano, Kata ya Mbwewe, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani, imepoteza maisha ya Mkurugenzi wa Benki ya ABSA na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Tawi la Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo kupitia taarifa yake iliyotolewa leo Alhamisi Agosti 3, 2023 na kusainiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutuma.

Katika taarifa hiyo, imesema kuwa ajali hiyo ilitokea jana Agosti 2, saa 2:30 usiku, ikihusisha gari aina ya Toyota Prado na Scania.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa gari ya Toyota Prado ilikuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, na kwamba ilikuwa ikiendeshwa na Nechi Msuya, huku Scania ilikuwa ikitokea Arusha na kwamba iliendeshwa na Philipo Mtisi.

Taarifa hiyo iliwataja waliofariki kwenye jali hiyo kuwa ni Nechi Msuya anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 45 hadi 50, Dayana Mageta, mfanyabishara na makazi wa Dar es Slaam anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 hadi 45, Nora Msuya anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 hadi 45 ambaye ni mwalimu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Tawi la Dar es Salaam, na abiria wa kike ambaye jina lake halikufahamika na anakadiriwa kuwa na miaka 30 hadi 35.

Polisi imeeleza chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Toyota Prado kuhama kutoka upande wa kushoto wa barabara kwenda upande wa kulia kisha kogongana uso kwa suo na lori hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: