Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Breaking News: Ajali yaua 18 Mafinga

Ajali Ajali Mafinga Watu 18 wafa ajali ya basi Mafinga

Fri, 10 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu 18 wamefariki dunia papo hapo baada ya basi dogo aina ya Costa kugongana uso kwa uso na lori la mizigo karibu na eneo la Changarawe, Mafinga mkiani Iringa.

Nae Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amethibitisha kutokea vifo hivyo akisema kuwa taarifa ziaidi zitatolewa baadaye

"Ni kweli ajali imetokea na inasadikika watu zaidi 10 wamepoteza maisha papo hapo," amesema.

Wakizungumza kwa njia ya simu baadhi ya watu walio katika eneo la tukio wamesema mpaka saa tatu asubuhi, jitihada za kuokoa majeruhi na kutoa miili ya watu zinaendelea.

Eneo ambalo ajali hiyo imetokea, ndilo ambalo basi la Majinja liliangukiwa na lori mwaka 2015 na kuua zaidi ya watu 40.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: