Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BREAKING: Ajali ya ndege Ziwa Victoria, Mwanza yazua taharuki - VIDEO

AJALI NDEGE TENAAA Ndege nyingine ya abiria yazama Ziwa Victoria

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ndege ndogo ya abiria ambayo bado haijajulikana ni kampuni gani inadaiwa kuanguka katika Ziwa Victoria leo Alhamisi, Februari 23, 2023 na kuzua taharuki huku chanzo cha ajali hiyo kikiwa hakijajulikana bado.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji tayari wamefika eneo la tukio na kuanza kutoa msaada ikiwa ni kuokoa abiria walikuwamo kwenye ndege hiyo kwa kushirikiana na wananchi wa eneo la karibu.

Kipande cha video ya tukio hilo kinaonyesha watu wakiokolewa majini huku ndege ikiwa imezama majini. Tayari magari ya kubeba wagonjwa yakipiga ving'ora yamefika eneo hilo na kubeba watu hao na kuwapeleka Hospitali.

Lakini inadaiwa kuwa huenda ni mazoezi ya uokoaji yanafanyika na Kikosi cha Uokoaji ili kujiweka tayari na matukio kama hayo endapo yakitokea.

Taharuki hiyo imetokea ikiwa ni miezi kadhaa tangu ajali ya ndege ya Shirika la Precision Air ilipoanguka katika Ziwa Victoria, Bukoba mkoani Kagera Novemba 6, 2022 na kuua watu 19, na kujeruhi 26 baada ya kushindwa kutua kutokana na hali mbaya ya hewa.

Tumefanya jitihada za kumtafuta Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza ili azungumzie tukio hilo lakini simu yake ya mkononi haipokelewi.

Aidha, taarifa ya mamlaka husika kuhusu tukio hilo bado haijatolewa. Endelea kufuatilia taarifa zetu kwa updates zaidi.

TAZAMA TUKIO HILO KWA KUBOFYA





TAA YAKANUSHA: HAKUNA AJALI YA NDEGE MWANZA

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: