Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya raia 1,000 wa EU wamesafirishwa kutoka Sudan

Zaidi Ya Raia 1,000 Wa EU Wamesafirishwa Kutoka Sudan Zaidi ya raia 1,000 wa EU wamesafirishwa kutoka Sudan

Mon, 24 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Zaidi ya raia 1,000 wa Umoja wa Ulaya walihamishwa kutoka Sudan mwishoni mwa juma huku kukiwa na mapigano makali kati ya makundi hasimu ya jeshi, mkuu wa sera za kigeni wa umoja huo Josep Borrell amesema.

Bw Borell aliwaambia waandishi wa habari kwamba ilikuwa operesheni ngumu lakini imefanikiwa - akiongeza kuwa balozi wa EU huko Khartoum bado yuko nchini.

Alisema kuwa Umoja wa Ulaya utaendelea na juhudi za kutafuta suluhu la kisiasa ili kumaliza mzozo ambao unaweza kuwa mbaya zaidi na kuleta athari katika bara zima la Afrika.

Uokoaji kutoka mji mkuu wa Sudan umeendelea usiku kucha, huku mapigano kati ya jeshi na kundi la wanamgambo la Rapid Support Group (RSF) yakiendelea.

Ufaransa, Ujerumani, Canada, Uhispania na Italia zote zimesema zimehamisha wafanyikazi wao wa kidiplomasia hadi mahali salama.

Zaidi ya watu 400 wameuawa na maelfu wengine kujeruhiwa, kulingana na UN.

Chanzo: Bbc
Related Articles: