Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri wa mambo ya ndani wa Sudan afutwa kazi

Waziri Wa Mambo Ya Ndani Wa Sudan Afutwa Kazi Waziri wa mambo ya ndani wa Sudan afutwa kazi

Tue, 16 May 2023 Chanzo: Bbc

Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amemfuta kazi kaimu waziri wa mambo ya ndani, Anan Hamed Mohammed Omar, ambaye pia ni mkuu wa polisi.

Katika taarifa yake, Jenerali Burhan alimtaja Khalid Hassan Muhyi al-Din kama mkurugenzi mkuu mpya wa polisi.

Hakuna sababu iliyotolewa ya kumfuta kazi lakini Jenerali Burhan awali alimfuta kazi kwa agizo kama hilo, gavana wa benki kuu na mawaziri wawili wa kigeni wanadiplomasia.

Poli imekuwa haifanyi kazi katika maeneo yaliyokumbwa na mzozo, ikiwa ni pamoja na mji mkuu, Khartoum, tangu mapigano yalipoibuka tarehe 15 Aprili. Matokeo yake, vitendo vya ukikaji wa sheria, ukiwemo uporaji na wizi, vimekuwa vikiripotiwakatika maeneo haya.

Mapiganno ya mwezi mmoja baina ya makundi hasimu ya kijeshi yanaonekana kutomalizika hivi karibuni kufuatia kuvurugika kwa mazungumzo ya amani yaliyoandaliwa na Marekani na Saudi Arabia.

Chanzo: Bbc
Related Articles: