Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri mkuu akanusha jeshi lake kupigana na Sudan

Bw Abiy Waziri mkuu akanusha jeshi lake kupigana na Sudan

Fri, 21 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed amekanusha ripoti kuwa jeshi la Ethiopia lilishambulia vikosi vya Sudan katika eneo la mpaka, na kuwaonya wanaoeneza taarifa hizo kuacha.

Bw Abiy alisema baadhi ya watu "walikuwa wakisambaza madai ya uongo ili kufanikiwa kisiasa wakati ambao watu wa Ethiopia na Sudan wanakabiliwa na changamoto nyingi".

“Tunalaani vikali madai haya ambayo yanalenga kuharibu uhusiano wetu wa kindugu na ujirani kati ya Ethiopia na Sudan,” Bw Abiy alisema hayo katika taarifa yake aliyoitoa kwenye Twitter.

Maoni ya waziri mkuu yanafuatia ripoti kwamba vikosi vya Ethiopia vilishambulia vikosi vya Sudan katika eneo linalozozaniwa la al-Fashaga, siku ya Jumanne, huku kukiwa na mapigano yanayoendelea kati ya vikosi hasimu nchini Sudan.

Sudan na Ethiopia zimekuwa katika mzozo mkali kuhusu eneo la al-Fashaga, ambapo Khartoum ilituma wanajeshi huko na kuchukua udhibiti wa sehemu kubwa ya eneo hilo mnamo 2021.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: