Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amekutana na Waziri Mkuu wa Sweden Ulf Kristersson mjini stockhom Alhamisi na kusema kuwa anatazamia kuiita Sweden ni mshirika wakati inajiandaa kujiunga na NATO.
Wote Sweden na jirani yake Finland waliomba kujiunga na NATO Mei mwaka 2022 kufuatia Russia kuivamia Ukraine.
Finland ilikuwa mwanachana wa 31 April 4 wa muungano huo mkubwa wa kijeshi, baada ya mabunge 30 ya taifa ya nchi wanachama wa NATO kuidhinisha uanachama wa taifa hilo la Nordic.
Maombi ya Sweden hata hivyo yamekwama kutokana na upinzani kutoka uturuki ambayo rais wake alisema nchi hiyo lazima itatue mizozo na stockhom.
Serikali ya uturuki imeishutumu Sweden kuwa mwepesi katika makundi yanayoonekana kuwa ya kigaidi.
Bunge la hungary nalo bado halijaipitisha Sweden kwenye ushirika wa NATO, na bado haiko bayana lini itafanya hivyo.
Kuna matumaini kwamba sweden itajiunga kabla ya Rais Joe Biden na wakuu wengine wa serikali wa NATO kukutana Vilnius, Lithuania mwezi July.