Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyakazi wa misaada washambuliwa Sudan kwenye mapigano

Wafanyakazi Wa Misaada Washambuliwa Sudan Kwenye Mapigano Wafanyakazi wa misaada washambuliwa Sudan kwenye mapigano

Wed, 19 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Mwandishi wa BBC aliyeko Khartoum, Mohamed Osman anasema mapigano yanaendelea katika baadhi ya maeneo ya mji huo yakiwemo makao makuu ya jeshi.

Ukubwa wa mapigano haujafahamika, lakini wakazi wa mji mkuu wa Sudan wanasema bado wanaweza kusikia milio mikubwa ya risasi.

Majenerali wawili hasimu, ambao wanajeshi wao wamekuwa wakipigania udhibiti, walikuwa wamekubali kusitishwa kwa mapigano ili kuruhusu misaada ya kibinadamu na raia kuondoka katika mapigano kwenda kupata misaada ya matibabu, lakini hilo halikutimia.

Mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa, Martin Griffiths, anasema wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wanashambuliwa na kunyanyaswa kingono.

Alisema ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Darfur Kusini imeporwa.

Mwandishi wa habari wa Sudan Muammar Ibrahim amesambaza picha hizi kutoka Nyala, Darfur Kusini, ambazo anasema zinaonesha soko lililoteketea na kuporwa majengo ya mashirika ya kimataifa:

Chanzo: Bbc
Related Articles: