Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umoja wa Mataifa kufanya kikao cha dharura kuhusu Sudan

Umoja Wa Mataifa Kufanya Kikao Cha Dharura Kuhusu Sudan Umoja wa Mataifa kufanya kikao cha dharura kuhusu Sudan

Thu, 11 May 2023 Chanzo: Bbc

Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa leo litafanya kikao cha dharura mjini Geneva siku ya Alhamisi, kujadili mzozo unaoendelea nchini Sudan.

Kuna ripoti za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mashambulizi dhidi ya raia, unyanyasaji wa kijinsia na uporaji wa hospitali.

Maelfu ya watu wamekimbia makazi yao na mashirika ya misaada yanasema hayawezi kufanya kazi kwa usalama.

Mataifa kadhaa ya Afrika, ikiwemo Sudan, yanaripotiwa kusitasita kuhusu mkutano huo unaofanyika, wakihofia kuwa unaweza kuhatarisha mazungumzo yanayoendelea ya kusitisha mapigano.

Kikao hicho kiliitishwa na Uingereza, Marekani, Ujerumani na Norway.

Chanzo: Bbc
Related Articles: