Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudani: Muda wa kusitisha mapigano umeongezwa, mapigano yanaendelea

Sudani: Muda Wa Kusitisha Mapigano Umeongezwa, Mapigano Yanaendelea Sudani: Muda wa kusitisha mapigano umeongezwa, mapigano yanaendelea

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Makundi ya kijeshi yanayohasimiana yamekubaliana kuongeza upya siku tatu za usitishaji mapigano, muda mfupi kabla ya kipindi cha awali kumalizika.

Kuongezwa- kwa muda wa saa 72 – kunafuatia juhudi kubwa za kudiplomasia za nchi Jirani, pamoja na Marekani, Uingereza na Umoja wa Mataifa.

Lakini kumekuwa na ripoti za kuendelea kwa mapigano makali katika mji mkuu Khartoum.

Mkataba wa awali uliwaruhusu maelfu ya watu kujaribu kukimbia , huku makumi kadhaa ya nchi zikijaribu kuwaokoa watu wake.

Mapigano ya wiki takriban mbili kati ya jeshi na kikundi hasimu cha kijeshi yamewauwa watu mamia kadhaa.

Muda wa kusitisha mapigano ulitarajiwa kuisha usiku, saa nne kwa saa za eneo(22:00 GMT).

Alhamisi usiku jeshi la Sudan lilikubali kuongezwa kwa muda huo, na baadaye mahasimu wao wa kikosi cha dharura- Rapid Support Forces (RSF) wakakubali kufanya hivyo.

Sudan Kusini imejitolea kupokea mazungumzo ya amani, na jeshi limekubali kutuma wawakilishi wake kwenye mazungumzo.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken samesema kuwa Washington ina "inafanya kazi kubwa" kuhakikisha kunakuwepo na mkataba wa usitishaji mapigano, na kuongeza kuwa licha ya kwamba sio mkamilifu umepunguza ghasia.

Lakini msemaji wa White House Karine Jean-Pierre baadaye alisema kuwa hali inaweza kuwa mbaya zaidi wakati wowote.

Wakati huo huo kundi RSF na mashahidi wanasema kuwa jeshi likipoteza maeneo yake katika mjini Khartoum.

Mapigano yamekuwa yakiripojtiwa katika jimbo la magharibi la Darfur na majimbo mengine.

Takriban watu 512 wameuawa katika mapigano huku 4,200 wakijeruhiwa, licha ya kwamba idadi halisi ya vifo inaweza kuwa kubwa zaidi.

Chanzo: Bbc
Related Articles: