Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan waadhimisha EID kwa mitutu ya bunduki

Sudan Vifooo Sudan waadhimisha EID kwa mitutu ya bunduki

Fri, 21 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vitongoji vya mji mkuu wa Sudan, Khartoum, vimeanza siku za kwanza za Idul Fitr kwa sauti za risasi na mabomu ya ndege za kivita na mizinga katika shambulio kubwa la Jeshi la Taifa kwenye viunga karibu vyote vya mji huo.

Kamandi ya Vikosi vya Jeshi la Taifa la Sudan imetangaza kwamba inaendesha operesheni ya nchi kavu katika jimbo lote la Khartoum, baada ya kile ilichokieleza kuwa ni "mafanikio ya oparesheni ya mashambulizi ya angani ambayo ililenga maeneo ya wapiganaji wa Kikosi cha Radiamali ya Haraka (RSF) mjini Khartoum alfajiri ya leo Ijumaa."

Ripoti zinasema mizinga ya RSF ilikabiliana na ndege za kivita za Jeshi la Taifa katika anga ya mji wa Khartoum, muda mfupi baada ya pande hizo mbili hasimu kutangaza makubaliano ya kusitisha mapigano wakati wa Sikukuu ya Idul Fitr, ambayo imenza leo Ijumaa nchini Sudan na katika baadhi ya nchi za Kiarabu na Kiislamu.

Jamii ya kimataifa imeendelea kuwasiliana na majenerali Abdel-Fattah al-Barhan na Mohammed Hamdan Daghlo maarufu kama Hamidati katika jitihada za kusitisha mapigano nchini Sudan ambayo hadi sasa yamesababisha vifo vya mamia ya watu. Khartoum

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametoa wito kwa pande zinazozozana nchini Sudan kuzingatia usitishaji vita wakati wa Sikukuu ya Idul-Fitr ili kuruhusu raia kufika maeneo salama, huku mapigano hayo yakiingia siku ya saba leo, Ijumaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: