Mwanafunzi mhandisi wa umeme mwenye umri wa miaka 27 amefariki akijaribu kurekebisha umeme katika hospitali iliyoathiriwa na mapigano katika jimbo la Darfur nchini Sudan
Muhammedin Fadul Idris Wadi, anayejulikana na marafiki zake kama Ala Danedn, alinaswa na umeme katika Kituo cha Afya cha Sayed al-Shahada katika jiji la Fasher siku ya Alhamisi.
Alikuwa sehemu ya kundi cha watu waliojitolea kujaribu kuendeleza kliniki huku kukiwa na makabiliano makali na uporaji.
"Alijulikana kwa tabasamu lake, hata wakati wa vita," rafiki yake alisema.
"Alitoa maisha yake kama mtumishi wa watu wa Fasher," Ahmed Ishaq, ambaye alisoma naye katika Chuo Kikuu cha Fasher, aliiambia BBC.
Ala Danedn alisifiwa kwa kazi yake ya kujitolea na mipango ya jamii aliyofanya bila ubinafsi, alisema.
Mstari wa lebo unaoambatana na picha yake ya wasifu kwenye Facebook unasema: "Usisubiri fursa, ibuni."
Tangu mzozo ulipozuka nchini Sudan kati ya makundi hasimu ya kijeshi tarehe 15 Aprili, kundi lake la watu wa kujitolea, linaloitwa Vijana wa Mpango wa al-Thawra, limejikita katika kusaidia matabibu huko Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini.
Vituo vyote vya matibabu vya Fasher, isipokuwa Hospitali ya Kusini - kliniki ya uzazi iliyorejeshwa - vilifufungwa kwa sababu ya kuwa karibu na eneo la mapigano, au wafanyikazi kutokwa na uwezo wa kuvifikia.
"Nilimwona akifanya kazi kwa bidii kuwasafisha na kupokea majeruhi katika Hospitali ya Kusini kaatika wiki nzima ya kwanza," alisema Bw Ishaq.