Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sehemu kubwa ya Sudan inasalia bila huduma za mtandao

Sehemu Kubwa Ya Sudan Inasalia Bila Huduma Za Mtandao Sehemu kubwa ya Sudan inasalia bila huduma za mtandao

Mon, 24 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Huduma za mtandao bado zinatatizika kote nchini Sudan huku mapigano kati ya jeshi na kikosi cha RSF yakiingia wiki ya pili, shirika la NetBlocks linaripoti.

"Sudan inasalia nje ya mtandao kwa kiasi kikubwa katikati ya kuzimwa kwa mtandao, huku asilimia 2% pekee ya ufikiaji wa mtndao kwa viwango vya kawaida ukiripotiwa" shirika hilo la kufuailia usalama wa mtandao lilisema katika taarifa.Jumatatu.

Imetaja madai ya kijeshi kwamba Vikosi vya RSF vinadaiwa kuhujumu mawasiliano ya simu katika mji mkuu Khartoum mapema Jumatatu, na kuathiri mitandao nchini humo.

Wakaaji wa Khartoum, hata hivyo, wanasema mawasiliamo yasimu bado yapo.

Mtandao wa kiraia ulioandaliwa hasa kupitia Twitter umekuwa ukitoa taarifa kuhusu mapigano hayo, hasa vidokezo kuhusu usaidizi unaopatikana na njia salama za kutoroka.

Mapigano nchini humo yamepelekea mataifa kadhaa kuwahamisha wanadiplomasia wao nchini humo.

Chanzo: Bbc
Related Articles: