Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Compaore ahukumiwa maisha jela kwa mauaji ya Sankara

Compaore Sankara.jpeg Rais Compaore ahukumiwa maisha jela kwa mauaji ya Sankara

Wed, 6 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Blaise Compaore; ni Rais wa zamani wa Burkina Faso ambaye Mahakama ya Kijeshi nchini humo imemuhukumu kifungo cha maisha gerezani kwa kuhusika katika mauaji ya mtangulizi wake, Thomas Sankara mwaka 1987.

Compaore ambaye yuko uhamishoni, amehukumiwa kifungo hicho bila kuwepo. Mkuu wake wa usalama, Hyacinthe Kafando pia amehukumiwa kifungo cha maisha jela.

Sankara; mwanamapinduzi aliyekuwa na itikadi za Ki-Marxist aliuawa kwa kupigwa risasi na kundi la watu wenye silaha katika Mji Mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou mwaka 1987.

Baada ya mauji hayo, Compaore alitawala kwa miaka 27 kabla ya kupinduliwa mwaka 2014.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: