Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wanakabiliwa na 'janga' huku 100,000 wakikimbia mapigano Sudan-UN

Raia Wanakabiliwa Na 'janga' Huku 100,000 Wakikimbia Mapigano Sudan UN Raia wanakabiliwa na 'janga' huku 100,000 wakikimbia mapigano Sudan-UN

Tue, 2 May 2023 Chanzo: Bbc

Zaidi ya watu 100,000 wameikimbia Sudan tangu mapigano makali yazuke kati ya vikosi hasimu tarehe 15 Aprili, Umoja wa Mataifa umesema.

Maafisa walionya kuhusu "janga kubwa" ikiwa mapigano hayataisha. Watu wengine 334,000 wamekimbia makazi yao ndani ya Sudan.

Mapigano yanaendelea katika mji mkuu, Khartoum, kati ya jeshi na kitengo pinzani cha wanajeshi wa RSF, licha ya kusitishwa kwa mapigano kutokana na kutekelezwa.

Siku ya Jumatatu, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Volker Perthes, aliliambia shirika la habari la AP kwamba pande hizo mbili zimekubali kushiriki mazungumzo ya kujadili usitishaji wa mapigano na kuleta "ulivu wa kudumu".

Saudi Arabia ilikuwa mahali pazuri pa mazungumzo, aliongeza. Ikiwa mazungumzo yatafanyika, itakuwa mkutano wa kwanza kati ya pande hizo mbili tangu mzozo huo uanze.

Zaidi ya watu 500 wameuawa na zaidi ya 4,000 wamejeruhiwa katika mapigano hayo, kwa mujibu wa wizara ya afya ya Sudan.

Msururu wa usitishaji mapigano kwa muda haujafanikiwa, huku jeshi likiendelea kuishambulia Khartoum kwa mashambulizi ya anga kwa nia ya kuidhoofisha RSF.

Mapigano makali pia yameshuhudiwa huko Darfur magharibi mwa Sudan.

Chanzo: Bbc
Related Articles: