Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege hazitaondoka Sudan baada ya vita itakaposimamishwa

Ndege Hazitaondoka Sudan Baada Ya Vita Itakaposimamishwa Ndege hazitaondoka Sudan baada ya vita itakaposimamishwa

Thu, 27 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Hakuna hakikisho kwamba ndege zaidi za uokoaji zitaondoka Sudan mara tu usitishaji wa mapigano utakapomalizika, waziri wa mambo ya nje ameonya.

Uingereza imesafirisha kwa ndege watu 536 kutoka nchi hiyo ya Afrika mashariki, na wengine wamewasili Uingereza.

Lakini hiyo ni sehemu ya maelfu ya raia wa Uingereza wanaodhaniwa kuwa katika nchi iliyokumbwa na migogoro.

"Hatuwezi kuhakikisha ni ndege ngapi zitaondoka mara tu usitishaji mapigano utakapokamilika," James Cleverly alisema Jumatano.

"Ikiwa unapanga kuondoka Sudan tafadhali safiri hadi kituo cha uokoaji cha Waingereza haraka iwezekanavyo."

Usitishaji vita wa saa 72, ambao ulikubaliwa na jeshi la Sudan na Kikosi cha (RSF), ulianza Jumanne lakini unamalizika Alhamisi saa sita usiku kwa saa za ndani (22:00 GMT).

Jeshi la Sudan lilisema lilikuwa tayari kutuma mwakilishi kwa mazungumzo kuhusu kurefusha muda huo, lakini hapajakuwa na majibu kutoka kwa RSF.

Marekani ilisema inawasiliana moja kwa moja na majenerali hao wawili wanaopigana ili kuona iwapo kipindi cha usitishaji mapigano kinaweza kurefushwa.

Tangu mapigano yalipozuka tarehe 15 Aprili, nchi hiyo imekumbwa na mzozo wa madaraka ambao umeshuhudia takriban watu 512 wakiuawa, kulingana na wizara ya afya ya Sudan, na maeneo ya makazi kugeuzwa kuwa maeneo ya vita.

Chanzo: Bbc
Related Articles: