Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzozo wa Sudan: Burhan amfuta kazi kiongozi wa kijeshi kama naibu wake

Sudan Pic Data Mzozo wa Sudan: Burhan amfuta kazi kiongozi wa kijeshi kama naibu wake

Fri, 19 May 2023 Chanzo: Bbc

Mkuu wa jeshi la Sudan Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amemfuta kazi makamu wake na kamanda wa Kikosi Maalum cha (RSF) Mohamed Hamdan Dagalo, maarufu Hemedti.

Jenerali Burhan na Hemedti wamehudumu kama mwenyekiti na naibu wa Baraza Kuu la utawala mtawalia, tangu mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba 2021.

Katika amri iliyotolewa Ijumaa, Jenerali Burhan alimteua aliyekuwa kiongozi wa waasi Malik Agar kuwa naibu wake. Bw Agar pia ni mjumbe wa Baraza Kuu.

Aliiagiza wasimamizi wa Baraza Kuu na mamlaka husika za serikali kutekeleza agizo hilo mara moja

Mwezi uliopita mkuu huyo wa jeshi alikivunja chama cha RSF na kuwateua wapiganaji wake kama waasi baada ya mzozo wa kuwania madaraka kuzuka kati ya vikosi pinzani.

Nchi hiyo tangu wakati huo imetumbukia katika mapigano mabaya na machafuko.

Chanzo: Bbc
Related Articles: