Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapigano yanapamba moto licha ya makubaliano ya kusitisha vita Sudan

Mapigano Yanapamba Moto Licha Ya Makubaliano Ya Kusitisha Vita Sudan.png Mapigano yanapamba moto licha ya makubaliano ya kusitisha vita Sudan

Thu, 27 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Mapigano yanaendelea katika baadhi ya maeneo ya Sudan licha ya kusitishwa kwa mapigano kwa saa .

Akizungumza kupitia simu kutoka Omdurman, mji unaopakana na mji mkuu Khartoum, mwandishi wa BBC Mohamed Osman anasema mapigano yalizuka karibu na majengo ya televisheni na redio.

Hakuna mafuta na kuna uhaba wa madaktari kuwahudumia watu na wengi wanatatizika kupata chakula na pesa, mwanahabari wetu anaongeza.

Mkuu wa jeshi la Sudan ameripotiwa kuidhinisha kurefusha muda wa usitishaji mapigano - unaotarajiwa kumalizika Ijumaa - kwa saa 72.

Jenerali Abdel Fattah al-Burhan alitoa idhini ya awali kwa pendekezo hilo kutoka kambi ya kikanda ya Afrika ya Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali, IGAD shirika la habari la Reuters linaripoti.

Pendekezo hilo linapendekeza kutuma wajumbe kutoka jeshi la Sudan na kundi pinzani la Rapid Support Forces (RSF) kwenda Juba nchini Sudan Kusini kujadili maelezo zaidi.

Usitishaji vita wa sasa ulianza usiku wa manane kwa saa za huko (22:00 GMT) siku ya Jumatatu na kuleta utulivu kwa mzozo huo uliozuka tarehe 15 Aprili huku kukiwa na mzozo wa madaraka kati ya viongozi wa jeshi na RSF.

Watu wa Khartoum na Omdurman wanapata shida kupata maji safi na chakula na kupata pesa taslimu, mwandishi wetu anasema.

Milipuko na milio ya risasi bado viliweza kusikika siku ya Jumatano, huku ndege za kivita zikiwa angani, ingawa kulikuwa na utulivu kuliko kabla ya usitishwaji wa mapigano na hali ilikuwa nzuri kiasi cha kuruhusu mpango wa kuwahamisha watu kuendelea.

Mwanahabari wetu anasema yeye na familia yake wanapata shida kulala kwa sababu ya milipuko na risasi.

Magenge pia yamekuwa yakipora nyumba na majengo matupu, yakilenga magari anaongeza. Wenyeji wanahofia kitakachotokea baada ya kumalizika kwa usitishaji mapigano

Chanzo: Bbc
Related Articles: