Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapigano Sudan: Wakazi wakimbia mji mkuu Khartoum

Mapigano Sudan: Wakazi Wakimbia Mji Mkuu Khartoum Mapigano Sudan: Wakazi wakimbia mji mkuu Khartoum

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Maelfu ya raia wameukimbia mji mkuu wa Sudan na mataifa ya kigeni yanajaribu kuwahamisha raia wao, huku kukiwa na mapigano makali ya siku ya sita.

Walioshuhudia waliripoti kuwa watu walikuwa wakiondoka Khartoum kwa magari na kwa miguu siku ya Jumatano asubuhi, huku milio ya risasi na milipuko ikitikisa jiji hilo.

Wakati huohuo, maafisa wa Japan na Tanzania wanasema wanafikiria kufanya mpango wa kuwahamisha raia wao. Msafara huo unafuatia kushindwa kwa usitishaji mapigano wa siku ya Jumanne kati ya pande zinazozozana.

Wanajeshi wa Sudan na Wanamgambo wa RSF walikuwa wamekubaliana kusitisha mapigano kwa saa 24 siku ya Jumanne, lakini mapatano hayo yalishindikana.

Usitishaji mpya wa mapigano kwa muda sawa ulitolewa na RSF siku ya Jumatano.

Jeshi lilisema litatii makubaliano hayo - lakini milio ya risasi bado inasikika katika mji mkuu.

Moshi ulionekana kwenye eneo la makao makuu ya jeshi katikati mwa jiji, ambako mapigano mengi kati ya makundi hasimu ya kijeshi yamejikita.

Mohammed Alamin, mwandishi wa habari aliyeko Khartoum, aliiambia redio ya BBC Focus on Africa kwamba milio ya risasi haikuacha, licha ya madai ya kusitisha mapigano.

"Inatisha sana - pande hizi zinazopigana zinafyatua risasi ovyo kila mahali," alisema.

"Niliona, mimi mwenyewe, mamia ya watu wakienda nje ya Khartoum, wakikimbilia katika majimbo jirani."

Baadhi ya raia hawakujua kilichokuwa kikitokea - huku wengine wakielekeza hasira zao pande zote mbili.

"Kimsingi watu wanafikiri kwamba vita hivi ni dhidi yao," Bw Alamin alisema.

"Hivi ndivyo watu waliniambia mitaani."

Pia alisema kuwa tatizo moja la kutekeleza usitishaji mapigano linaweza kuwa ni vikosi vilivyogawanyika katika jiji hilo.

"Kuna aina ya utengano kati ya askari hawa - wanapigana katika maeneo tofauti na mawasiliano kidogo ...," alisema. Mapigano hayo kwa sasa yanahusisha zaidi kurusha makombora na si mashambulizi ya mabomu ya angani.

Chanzo: Bbc
Related Articles: