Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapigano Sudan: Hospitali 39 'zimepigwa mabomu'

Wafanyakazi Wa Misaada Washambuliwa Sudan Kwenye Mapigano Mapigano Sudan: Hospitali 39 'zimepigwa mabomu'

Wed, 19 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Muungano wa madaktari wa Sudan umesema kuwa hospitali 39 kati ya 59 katika mji mkuu, Khartoum na majimbo ya jirani "hazina huduma", na kuangazia hali mbaya ya kibinadamu nchini humo.

Kamati kuu ya madaktari wa Sudan (CCSD) ilisema katika taarifa yake kwenye Facebook siku ya Jumatano asubuhi kuwa ni hospitali 20 pekee ndizo zinazofanya kazi kikamilifu au kwa kiasi.

"Kati ya hospitali ambazo zimeacha kufanya kazi, kuna hospitali tisa ambazo zililipuliwa na hospitali 16 ambazo zililazimika kuhamishwa," CCSD ilisema.

Mapigano yanaendelea Khartoum na maeneo mengine ya Sudan huku jeshi na jeshi la wanamgambo wakilaumu kukiuka mapatano ya kibinadamu ya saa 24 ambayo yalikuwa yaanze kutekelezwa Jumanne jioni.

Chanzo: Bbc
Related Articles: