Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapigano Sudan : Hali ya hivi punde kabisa nchini

Mapigano Sudan : Hali Ya Hivi Punde Kabisa Nchini Mapigano Sudan : Hali ya hivi punde kabisa nchini

Sat, 29 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Licha ya kuongezwa rasmi kwa muda wa usitishaji mapigano wa saa 72 nyingine, mapigano nchini Sudan yameingia wiki ya tatu.

Khartoum: Mji mkuu wa Sudan umekuwa ukipigwa na mashambulio ya anga, vifaru na makombora. Jeshi la Sudan limekuwa likituma ndege aina ya jet au dronikwa mahasimu wao wa vikosi vya dharura- Rapid Support Forces (RSF), katika maeneo jirani mbali mbali katika mji mkuu, na hivyo kusababisha hali kuwa mbaya zaidi kwa wakazi ambao wana kiasi kidogo cha umeme, mafuta, maji na chakula.

Miji iliyopo karibu na Khartoum: Mapigano yanaendelea katika miji iliyopo karibu na mji mkuu Khartoum, mkiwemo Bahri na Ombdurman, kulingana na shirka la habari la Reuters. Katika Omdurman, vikosi vya RSF vimeripotiwa kushutumu jeshi kwa kuvunja mkataba kwa mashambulio kwenye ngome zake zilizo mjini.

Darfur: Katika jimbo la magharibi la Darfur, jiji la El Geneina limeshuhudia wapiganaji wakipora na kuchoma nyumba na benki. Madaktari wanasema takriban watu 74 wameuawa katika mashambulizi pale wiki hii. Maelfu ya watu wanatoroka jimbo hilo na kuvuka mpaka wakiingia Chad.

Chanzo: Bbc
Related Articles: