Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapigano Sudan: Hali bado tete, milio ya risasi yaendelea kurindima

Wafanyakazi Wa Misaada Washambuliwa Sudan Kwenye Mapigano Mapigano Sudan

Wed, 19 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miripuko ya risasi na mabomu, imeendelea kusikika katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum licha ya upande mmoja kudai kusitisha mapigano yaliodumu kwa siku ya nne ambayo yamesababisha vifo vya karibu watu 200.

Mapambano hayo ya kuwania madaraka, yalizusha mapigano kati ya vikosi vya majenerali wawili walionyakua mamlaka katika mapinduzi ya 2021, yaani mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake, Mohamed Hamdan Dagalo, ambaye anaongoza Kikosi cha Msaada wa Dharura, RSF.

Hatua hiyo, imepelekea wito wa kimataifa wa kukomesha uhasama uliosababisha kuongezeka kwa uasi, vifo na uharibifu huku Kamanda wa RSF, Dagalo, anayejulikana kama Hemeti, akitangaza kuunga mkono jitihada ya kimataifa ya kusitisha mapigano kwa masaa 24 huku upande wa jeshi la Sudani ukionekana kama kutotilia maanani jambo hilo.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema hadi sasa mapigano nchini Sudan, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Khartoum na maeneo mengine mbalimbali hayana dalili ya kusitishwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: