Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kundi la kwanza la raia wa Kenya laondolewa Sudan

Kundi La Kwanza La Raia Wa Kenya Laondolewa Sudan Kundi la kwanza la raia wa Kenya laondolewa Sudan

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Kundi la kwanza la Wakenya kutoka Sudan iliyokumbwa na vita limewasili Nairobi kwa ndege ya kijeshi Jumatatu usiku.

Kundi hilo lilikuwa na Wakenya 19, Wasomali 19 na raia mmoja wa Saudi Arabia ambao wote walisafiri kwa barabara hadi Sudan Kusini ambako walipanda ndege hiyo ya kivita.

Waziri wa Ulinzi Aden Duale, alisema wote walikuwa wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha kimataifa nchini Sudan.

"Ninawapongeza watu hawa kwa kufanya safari ndefu na ninashukuru timu zinazohusika katika kuwezesha harakati zao. Serikali imejitolea kuhakikisha kuwa Wakenya wanarejea salama kutoka Sudan," alisema Duale.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni Alfred Mutua alishukuru nchi zilizowaruhusu Wakenya kuvuka mipaka kutoka Sudan na kuruhusu ndege za Kenya kuruka juu ya anga zao kutekeleza zoezi hilo.

Wakimbizi zaidi watasafirishwa kwa ndege hadi Nairobi siku zijazo na timu ya maafisa wa kijeshi ambao wanaongoza zoezi hilo kwa ushirikiano na maafisa wa Masuala ya Kigeni.

Serikali hiyo tayari imetambua Wakenya 3,000 nchini Sudan na inawataka wanaohitaji kuhamishwa kusajili majina yao, maeneo na nambari zao za pasipoti kwenye simu za dharura ili mipango muhimu ifanywe.

Kundi linalofuata la wahamishwaji litajumuisha kundi la wanafunzi 29 waliovuka mpaka na kuingia Ethiopia baada ya kutoroka Sudan.

Chanzo: Bbc
Related Articles: