Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi vita ya Sudan: Hatutafanya mazungumzo hadi mapigano yaishe

Kiongozi Vita Ya Sudan: Hatutafanya Mazungumzo Hadi Mapigano Yaishe Kiongozi vita ya Sudan: Hatutafanya mazungumzo hadi mapigano yaishe

Sat, 29 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Mmoja wa majenerali wawili, wanaoongoza kikosi cha dharura kinachopigana dhidi ya jeshi la nchi nchini Sudan, ameiambia BBC kwamba hatafanya mazungumzo mpaka mapigano yaishe.

Lakini Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, anayefahamika zaidi kama Hemedti, amesema kuwa wapiganaji wake wanapigwa "bila kuchoka" mabomu tangu mkataba wa siku tatu wa kusitisha mapigano uongezwe.

"Hatutaki kuiangamiza Sudan," alisema, akimlaumu mkuu wa majeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan kwa ghasia.

Jenerali Burhan amekubali kufanya mazungumzo ya ana kwa ana katika Sudan Kusini.

Urefushaji wa muda wa usitishaji mapigano ulifikiwa Alhamisi usiku kufuatia juhudi kubwa za kidiplomasia za nchi jirani, pamoja na Marekani, Uingereza na Umoja wa Mataifa.

Akizungumza na BBC kwa njia ya simu, Hemedti alisema kuwa yuko tayari kwa mazungumzo lakini kwa sharti kwamba usitishwaji wa mapigano unaheshimiwa:

"Acha uhasama. Baada ya hapo tunaweza kuwa na mazungumzo."

Alisema kuwa hana tatizo la kibinafsi na Jenerali, lakini anamchukulia kama msaliti kwa kuwaleta ndani ya serikali wale waliokuwa watiifu kwa rais wa zamani Omar al-Bashir, ambaye alipinduliwa na jeshi na RSF pamoja mwaka 2019 baada ya maandamano makubwa ya mitaani.

Utawala wa Bashir – ambao umekuwa madarakani kwa miongo mitatu – ulifahamika kwa itikadi zake kali za Kiislamu na kuweka masharti makali ya Sharia (Sheria ya Kiislamu).

"Kwa bahati mbaya Burhan anaongozwa na Waislamu viongozi wenye itikadi kali wa Kiislamu," Hemedti alisema.

Mnamo mwaka 2021, yeye na Jenerali Burhan walikataa makubaliano ya kugawana madaraka na raia, na kuchukua udhibiti kamili wa mapinduzi.

Walikosana mwaka huu kuhusu pendekezo la kurejesha mamlaka ya uongozi wa kiraia, hususan muda wa kuwajumuisha wanajeshi wa kikosi imara cha Hemedti cha wanajeshi 100,000- wanaounda kikosi cha dharura- Rapid Support Force's (RSF) katika jeshi.

"Ninatamani kuwa na serikali ya kiraia leo – kabla ya kesho, serikali kamili ya kiraia. Huu ndio msimamo wangu," Hemedti aliiambia BBC.

Hii si mara ya kwanza kwa kiongozi wa RSF kuzungumzia kuhusu kujitolea kwake kuhakikisha kunakuwa na demokrasia nchini Sudan, ingawa wachambuzi wanasema kwamba kikosi chake kimekuwa kikitumia kukatili kuzuia maandamano ya raia awali.

Hemedti aliiambia BBC kwamba wapiganaji wa RSF sio maadui wa wanajeshi, akielezea kuwa wanapigana kulinda nchi dhidi ya "mabaki ya serikali ya miaka 30 iliyopita."

"Hatutapigana na nyingi. Tafadhali nendeni kwenye vitengo vyenu vya kijeshi na hatutapigana nanyi."

Kauli za Hemedti kwa BBC zinakuja huku mamilioni ya watu wakiendelea kukwama katika mji mkuu Khartoum, ambako kuna uhaba wa chakula, maji na mafuta.

Katika baadhi ya maeneo ya mji, mitaro imekuwa ikichimbwa huku wanajeshi wakipigana wenyewe kwa wenyewe mtaa kwa mtaa, linasema shirika la habari la AFP.

Umoja wa Mataifa unasema vikosi vya RSF vinawalazimisha watu kuzikimbia nyumba zao na uporaji na unyang’anyi vinaendelea.

Hatahivyo, Hemedt, ameiambia BBC kuwa mahasimu wake wanavaa mavazi magwanda ya RSF ili kuwashushia hadhi.

Alipinga vikali kuhusuika kwao katika uporaji na kuteka hospitali, akisema kuwa wanajeshi wake walikuwa wanajaribu kuwasaidia wakazi wa mji wanaokimbia mapigano yaliyodumu kwa siku 14.

"Timu yangu inafanyia kazi mifumo ya kusambaza maji kwa ajili ya maeneo tunayoyadhibiti. Kwa bahati mbaya mafundi wote na wahandisi wametoweka. Na hili ni tatizo letu kuu," alisema.

Takriban watu 512 wameuawa na wengine 4,193 wamejeruhiwa, kulingana na takwimu za wizara ya afya, ingawa idadi kamili ya vifo inaweza kuwa juu zaidi.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa maelfu kwa maelfu ya Wasudan sasa wamezikimbia nyumba zao, mara nyingi wakilazimika kulipa pesa nyingi kuondoka na kukabiliwa na unyanyasaji wanapokuwa njiani.

Pamoja na maelfu ya raia wa kigeni ambao wameokolewa, maelfu ya Wasudan wamevuka mipaka na kuingia nchi jirani, zikiwemo Chad, Misri na Sudan Kusini.

Shirika la habari la Reuters linaripoti kuwa Umoja wa Mataifa unasema baadhi wametembea kutoka Sudan Khartoum hadi kwenye mpaka wa Sudan Kusini, umbali wa zaidi ya kilomita 400 (maili 250).

Awali, ndege ya uokozi ya Uturuki ilipigwa risasi, wakati ilipokuwa ikitua katika uwanja wa ndege uliopo nje ya mji wa Khartoum. Hakuna aliyejeruhiwana RSF ilikanusha shutuma za jeshi kwamba ilihusika na shambulio hilo.

Wale waliobaki katika mji wa Khartoum wanaelezea kuishi "maisha ya uoga wakati wote."

"Tunasikia sauti za ndege na milipuko. Hatujui ni lini maisha haya mabaya yatamalizika," Mahasin al-Awad, mwenye umri wa miaka 65, makazi wa Bahri, kaskazini mwa mji wa Khartoum, aliimbia Reuters.

Ghasia zimeripotiwa kuwa mbaya zaidi hususan katika El Geneina, mji wa Darfur uliopo magharibi mwa Sudan, ambako RSF na wanamgambo wenye uhusiano kikundi hicho wameripotiwa kupora na kuchoma moto masoko, maghala ya chakula na benki.

Chanzo: Bbc
Related Articles: