Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye mwili wa mzee aliyekaa mochwari miaka 6 kuzikwa

Jeneza Mwili M Hatimaye mwili wa mzee aliyekaa mochwari miaka 6 kuzikwa

Mon, 25 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miezi michache iliyopita palizuka mtafaruku baada ya familia moja kaunti ya Kisii ambao walishindwa kumzika mpendwa wao kutokana na mzozo wa ardhi ambapo mtu mmoja alijitokeza na kudai mzee huyo wa familia (marehemu) alikuwa amekufa alimuuzia shamba lake lote na hivyo kuzuia mwili wake kuzikwa katika eneo hilo.

Katika kisa hicho, kilichoripotiwa na vyombo vya habari nchini Kenya, mzee huyo alifariki na kulazimu mwili wake kusalia katika chumba cha kuhifadhi maiti kwa zaidi ya miaka sita huku kesi ya mzozo wa ardhi baina ya familia yake na mtu aliyedai kuuziwa shamba hilo ikiendelea kortini miaka hiyo yote.

Inasemekana mzee huyo kwa jina Oribo kutoka maeneo ya Kiamokana kaunti ya Kisii aliuza shamba lake mwaka 1969 na alipofariki miaka 6 iliyopita, mwenye shamba ambaye alinunua na kumpa Oribo na familia yake idhini ya kuendelea kukaa kwenye shamba hilo alizuka na kudai shamba lake pasizikwe mtu.

Baada ya familia hiyo kuhaingaika kwenye milango ya mahakama kwa miaka sita, hatimaye wamesalimika baada ya Waziri wa usalama Dkt. Fred Matiang’i kuingilia kati na kutatua mgogoro huo ambapo familia hiyo imeruhusiwa kumzika mpendwa wao baada ya kubainika kwamaba mzee huyo hakuuza shamab lake lote kama ambavyo mlalamishi alikuwa anadai bali ni sehemu kidogo tu.

Siku chache zilizopita wakati Waziri Matiang’i alikuwa kweney mahojiano ya kipekee na kituo kimoja cha redio humu nchini, watu wengi walimtaka kuzungumzia suala hilo ambapo aliahidi kuingilia kati ili familia hii ipate haki, ahadi ambayo alitimiza siku chache baadae. Matiang’i pia aliahidi kuwajengea wanafamilia hii nyumba katika sehemu ya shamba ambalo lilibaki.

Katika picha ambazo zilipakiwa mitandaoni, inasemekana Waziri Matiang’i hatimaye aliwajengea wanafamilia hao nyumba mbili na mzee Oribo anatarajiwa kupumzishwa leo hii baada ya kukaa mochwari kwa miaka sita.

Mzozo huo ulizuka baada ya wanaharakati na watetezi wa haki za kibinadamu wakiongozwa na Samwel Okemwa ambaye analenga kuwa seneta wa kaunti hiyo, kuingilia kati na vyombo vya habari kuliangazia Sakata la familia hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: