Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna suluhu ya Sudan hadi wapiganaji waondoke mji mkuu - jeshi

Hakuna Suluhu Ya Sudan Hadi Wapiganaji Waondoke Mji Mkuu   Jeshi Hakuna suluhu ya Sudan hadi wapiganaji waondoke mji mkuu - jeshi

Mon, 5 Jun 2023 Chanzo: Bbc

Naibu mkuu wa baraza tawala la Sudan, Malik Agar, amekaribisha mazungumzo ya kusitisha mapigano zaidi lakini akasema hakuna mapatano yanayoweza kudumu hadi majeshi yote yaondolewe katika mji mkuu.

Kumekuwa na ongezeko la kutisha la ghasia mjini Khartoum na katika eneo la magharibi la Darfur tangu mazungumzo nchini Saudi Arabia yalipovunjika wiki iliyopita.

Jeshi na kikosi pinzani cha wanamgambo, Rapid Support Forces (RSF), walishutumu kila mmoja kwa kukiuka mapatano hayo, lakini wapatanishi wamesalia Jeddah.

Bw Agar alisema mazungumzo hayo yanawakilisha matumaini bora ya kukomesha mapigano.

Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan hivi majuzi alimteua Bw Agar, kiongozi wa zamani wa waasi, kuchukua nafasi ya makamu wake wa zamani Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana pia kama Hemedti, ambaye anaongoza RSF.

Wanajeshi wengi huko Khartoum ni wapiganaji wa RSF, na jeshi linaonekana kuanza tena majaribio yake ya kuwaondoa katika nafasi wanazoshikilia.

Chanzo: Bbc
Related Articles: