Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna haja ya mazungumzo bila usitishaji wa mapigano - Burhan

Hakuna Haja Ya Mazungumzo Bila Usitishaji Wa Mapigano   Burhan Hakuna haja ya mazungumzo bila usitishaji wa mapigano - Burhan

Tue, 9 May 2023 Chanzo: Bbc

Taarifa zinaendelea kutolewa hadharani kuhusu yanayoendelea katika mazungumzo ya upatanishi wa Sudan unaongozwa na Saudi Arania na Marekani huko Jeddah kati ya Jeshi la Sudan (SAF) na Kikosi Maalum cha Sudan (RSF) yaliyoanza tarehe 6 mwezi Mei.

Lakini kiongozi wa SAF Jenerali Abdel Fattah al-Burhan Jumatatu aliambia Televisheni ya Al-Qahera News ya Misri kwamba "hakuna manufaa yoyote ya kukaa kwenye meza ya mazungumzo nchini Saudi Arabia" bila ya usitishaji mapigano wa kweli.

Jenerali Burhan alisema anakaribisha mipango yote ambayo inalenga kukomesha umwagaji damu lakini kusisitiza kuwa RSF lazima iweke sila chini.

Mwanadiplomasia wa Saudia awali aliliambia shirika la habari la AFP kwamba majadiliano hayajazaa matunda "hakuna hatua kubwa" iliyopigwa.

Mikakati mingi ya kusitisha mapigano imekiukwa tangu mzozo huo kuzuka tarehe 15 Aprili.

Chanzo: Bbc
Related Articles: