Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna dalili ya RSF kukimbia makombora - wakazi wa Khartoum

Maelfu Ya Wakimbizi Wa Sudan Kukutana Na Mkuu Wa USAID Hakuna dalili ya RSF kukimbia makombora - wakazi wa Khartoum

Sat, 3 Jun 2023 Chanzo: Bbc

Wakazi wa mji mkuu wa Sudan Khartoum, wameripoti mapigano makali kati ya jeshi na wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF).

Haya yanajiri licha ya vikwazo vya Marekani vilivyowekwa baada ya kuvunjika kwa juhudi za usitishaji mapigano.

Watu katika jiji hilo walisema jeshi lilianza tena mashambulizi ya anga na lilikuwa likitumia mizinga zaidi, lakini bila dalili kwamba RSF inajiondoa mitaani na nyumba walizokalia.

Jeshi lilitangaza kuimarisha uwepo wao katika mji mkuu kutoka maeneo mengine ya Sudan.

Wachambuzi wanasema vikosi vya jeshi vinatarajiwa kufanya mashambulizi makubwa ili kuwaondoa wanamgambo hao mitaani.

Chanzo: Bbc
Related Articles: