Fri, 21 Apr 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Antonio Guterres, ametoa wito kwa pande zinazohasimiana nchini Sudan, kusitisha mapigano katika kipindi hiki cha Eid al-Fitr, ili kuwaruhusu raia kufika maeneo salama.
Na wakati huu maelfu ya raia wakitafuta nanmna ya kukimbia mapigano katika mji mkuu wa Khartoum, inaripotiwa kuwa takriban raia elfu 4 kutoka nchi za Afika Mashariki wamekwama nchini Sudan.
Hapo jana, mapiganao kati ya jeshi la Sudan na vikosi vya RSF yaliendelea kwa siku ya sita, wakati huu maelfu ya raia wakiripotiwa kuvuka mpaka na kuingia nchini Chad.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: