Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulinzi waimarishwa kuelekea Kariakoo Dabi

Muliro Jumanne Marufuku Ulinzi waimarishwa kuelekea Kariakoo Dabi

Fri, 18 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Mliro amesema jeshi la Polisi limejipanga kuimarisha ulinzi kwenye mchezo wa kesho wa ligi Kuu ya NBC kati ya Simba na Yanga.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mliro amesema hakuna mtu yeyeto atakayeruhusiwa kuingia na silaha zaidi ya Askari Polisi ambao watakuwa kwenye zamu.

Aidha ameongeza kuwa magari yote yatakayo ruhusiwa kuingia uwanjani ni yale yenye kadi maalum huku akisema njia za kuingilia uwanjani hapo na kutoka zitakuwa na ulinzi ili wananchi wapite kwa usalama zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: