Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fadlu: Dabi ni ngumu ila haiwezi kuamua Ubingwa

Fadlu D Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids

Fri, 18 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amesema mchezo wa kesho Kariakoo derby dhidi ya Yanga hauwezi kuamua ubingwa.

“Ni mechi muhimu sana kwa sababu timu zote zinaangaliwa sana, ni mechi muhimu sana kwenye ligi lakini haitaamua ubingwa wa ligi”

Aidha Fadlu ameongeza kuwa Yanga wamekua na timu yao kwa kipindi cha miaka mitatu na wamefanikiwa kutwaa ubingwa mara tatu lakini wanawapa heshima yao ila wanajua namna gani ya kucheza nao.

“Tumefuatilia mechi zao na tunawafahamu jinsi wanavyoenda kucheza mechi zao na tumefanyia kazi, kiwango na historia kwenye mechi hizi hazina nafasi sana kwa sababu kwenye derby timu itakayokua bora ndiyo itashinda mechi.”

Unaona mchezo wa Derby ya Kariakoo ukiamua nani kuwa bingwa 2024/25?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: