Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simai aeleza urafiki wake na Lowassa, vyakula alivyopenda

Simai Mohamed Said Pic Simai aeleza urafiki wake na Lowassa, vyakula alivyopenda

Tue, 13 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama ulikuwa haujuii, Simai Mohamed Said ni miongoni mwa marafiki wa Waziri Mkuu mstaafu, hayati Edward Lowassa na ameeleza jinsi alivyofahamiana naye.

Simai, mwakilishi wa Tunguu mkoani Kusini Unguja, ameeleza hayo leo, Februari 13, 2024 alipozungumza na Mwananchi Digital katika shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Lowassa aliyefariki dunia Februari 10, mwaka huu.

Amesema nyumbani kwake ndiko Lowassa alikokuwa akifikia mara nyingi alipokwenda visiwani humo hasa mwaka 2015.

Simai aliyejiuzulu wadhifa wa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Januari 25, mwaka huu, amesema walifahamiana na Lowassa tangu miaka ya 1990 kipindi ambacho alichokuwa akisoma shule moja na mtoto wa Lowassa, Fred Lowassa (Mbunge wa Monduli).

"Uhusiano wangu na mzee Lowassa ni wa kifamilia na nilikuwa mtu wake wa karibu katika mambo ya siasa hasa mbio za urais mwaka 2015," amesema.

Kwa mujibu wa Simai, ushawishi wa mwanasiasa huyo na mapenzi yake kwa vijana ndiyo ulioongeza ukaribu wao.

Amesema mikutano mingi ya mwanasiasa huyo katika mbio za urais mwaka 2015, alikuwa anafanya nyumbani kwa Simai.

Alivyopenda pilau, mbuzi

Katika vitu anavyovikumbuka kwa rafiki yake huyo ni kile alichoeleza, alipenda pilau, nyama ya mbuzi na maziwa.

"Alipokuwa anakuja nyumbani alikuwa anapenda kula pilau na nyama ya mbuzi. Kwa hiyo tulikuwa tunamuandalia chakula chake na chai ya maziwa alikuwa anajisikia raha sana," amesema Simai.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: