Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fredy Lowassa: Asingekuwa Rais Samia, baba asingefika juzi

Lowassa X Mke X Samia Lowassa na Rais Samia.

Tue, 13 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Jimbo la Monduli, ambaye ni mtoto wa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Lowassa, aitwaye Fredrick Edwad Lowassa amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa msaada mkubwa kwa familia hiyo kuhakikisha afya ya mzee huyo ina imarika lakini Mungu aliamua vingine.

Fredy amesema hayo leo Jumanne, Februari 13, 2024 kwenye Ukumbi wa Karimjee wakati akitoa salam za rambirambi katika zoezi la kuaga mwili wa marehemu baba yake aliyefariki Dunia Jumamosi iliyopita katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Muhimbili Dar.

"Baba ni mpambanaji alipambana sana mpaka dakika ya mwisho lakini kwa yaliyotokea tunasema ni kazi ya Mungu na kama familia tulipokea kwa amani kabisa, tunasema acha baba apumzike.

"Lakini katika vita yake hii ya kupigania maisha yake lazima niseme kipekee naomba sana kutoa shukrani za familia kwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

"Niseme ukweli kutoka moyoni, kama isingekuwa mama Samia Suluhu Hassan, baba yetu asingefika hata hiyo juzi, mama Samia amekuwa ni ndugu, amekuwa mzazi na mlezi wetu hatuna cha kumlipa," amesema Fredrick Edwad Lowassa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: