Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugu wa Magufuli: Niko tayari kutangulia mbele za haki

Video Archive
Sat, 7 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa dada wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aitwaye Furaha Dominic amesema yupo tayari kutangulia mbele za haki lakini hayuko tayari kuona Watanzania wenzake wananyanyaswa.

Furaha amesema hayo wakati akifanya mahojiano na Global TV Online katika kipindi maalum cha Hoja kwa Hoja huku akieleza kuwa kiongozi huyo hakuwa mkali kama baadhi ya watu ambavyo wamekuwa wakimtafsiri.

“Siasa ni kutafuta dhamana ya kuwaongoza na kuwasaidia watu. Siamini katika siasa ya kuuwana, watu wanaokuua ni watu walewale wa karibu, mtu asiyekujua hawezi kukudhuru.

“Nimegundua kwenye siasa unapoanza kutetea watu unatengeneza adui na watu kwa sababu wanafaidika kutokana na matatizo ya watu. Kwa hiyo linapokuja suala la mtu kunyanyaswa, nipo tayari kutangulia mbele za haki ili kumtetea huyo mtu.

“Mimi ni Mtanzania, nina haki zote za kuishi na kuheshimiwa katika nchi yangu. Mimi sikuwa naishi kwa sababu ya Hayati Magufuli, yeye alikuwa Rais wa Tanzania.

“Kwa sasa nina Amani kuliko hata Kipindi cha Magufuli kwa sababu wakati ule nilikuwa nikifanya chochote utasikia anafanya hivyo kwa sababu ni ndugu wa Rais Magufuli. Hata ukinipiga mimi au ukanidhuru tukaenda polisi sina haki, itaonekana kwa sababu ni ndugu wa Rais,” amesema Furaha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: