Mpwa wa dada wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aitwaye Furaha Dominic amekiri kuwa alifukuzwa kazi siku chache tu mara baada ya kifo cha kiongozi huyo aliyeaga dunia Machi 17, 2021.
Furaha amesema hayo wakati akifanya mahojiano na Global TV Online katika kipindi maalum cha Hoja kwa Hoja huku akieleza kuwa kiongozi huyo hakuwa mkali kama baadhi ya watu ambavyo wamekuwa wakimtafsiri.
"Siasa ni tamu, ukiwa mchanga itakuumiza ila ukikomaa utazoea, unaweza kuwa unafanya kazi vizuri sana ukawa kama Malaika ila ukiingia kwenye siasa tu unakuwa mbaya.
"Ni kweli mimi nilipata changamoto mara tu baada ya kifo cha Rais Magufuli, lakini nilikuwa na subira na nilifuata taratibu za utumishi wa umma. Yani mtu anakwambia tu hukuwepo ofisini mwezi Januari Zaidi ya siku tano.
"Lakini amesahau kama alikutuma sehemu flani. Mimi nilianza kuonekana mbaya baada tu ya siasa. Sina kashfa ya kupokea wala kutoa rushwa, nilikuwa na ukamilifu wa mtu aliyenyooka kazini.
"Niilifuata taratibu za kiutumishi na sasa nimerudishwa kazini. Suala la mimi kufanya siasa hata Hayati Magufuli hakupenda kabisa, limeniletea changamoto nyingi kwenye familia yangu.
"Lakini leo hii hata nikisema mimi sio mwanasiasa hakuna atakayeamini, wala watesi wangu hawataamini maneno yangu," amesema Furaha.