Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Gamondi amesema ameanza kuona dalili za ubingwa kufuatia kiwango bora ambacho kimeoneshwa na timu yake ka tika mchezo wa juzi Jumatatu (Oktoba 23) dhidi ya Azam FC.
Young Africans ipo kileleni mwa msimamo hivi sasa wakifikisha pointi 15 sawa na Simba SC lakini mabingwa hao watetezi wapo mbele kwa mchezo mmoja.
Kocha huyo amesema wachezaji wake walionesha tabia halisi za timu bingwa na wanahitaji ubingwa msimu huu kutokana na kucheza kwa kujitoa na kutafuta pointi tatu licha ya kutanguliwa.
“Nilitarajia ugumu kwenye mchezo ule, wachezaji wangu wameonesha tabia halisi ya kwamba wapo kwenye timu kubwa inayohitaji ubingwa, tulicheza vizuri kipindi cha pili licha ya kutanguliwa bao la Penati lakini tulipambana na kusawazisha makosa yetu,” amesema Gamondi.
Kocha huyo pia alimpongeza mfungaji wa mabao yote matatu Stephen Aziz Ki, akisema ni mchezaji wa daraja la juu mno na pamoja na uchovu aliokuwa nao lakini alicheza kwa kujitoa kuipigania timu yake kitu ambacho kimeonesha ana mapenzi makubwa na timu hiyo.
Naye Kocha Msaidizi wa Azam FC, Bruno Ferry amesema kilichowaangusha kushindwa kudhibiti mchezo baada ya kuongoza 2-1 kutokana na kukosa uzoefu kwa wachezaji wake dhidi ya ubora waliokuwa nao wachezaji wa wapinzani wao Young Africans.
Amesema ulikuwa mchezo mkubwa uliokutanisha timu mbili kubwa na walijitahidi kupambana kwa kuushika mchezo katika baadhi ya nyakati lakini ubora wa Young Africans hasa kiungo Aziz Ki ndio uliwaletea shida na kujikuta wanapoteza mchezo.
“Naipongeza Young Africans pamoja na Azizi Ki, alikuwa bora na ndio amesababisha tukapoteza mchezo lakini ndio mpira tunarudi kujipanga ili kufanya vizuri mchezo unaokuja lengo ni kubeba ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu” amesema Ferry.
- Serikali yataifisha Tanzanite, yafunga mgodi
- Mpwa wa Magufuli 'amchimba mkwara' Askofu Gwajima
- Mpwa wa Magufuli akiri kufukuzwa kazi baada ya kifo cha JPM
- Ndugu wa Magufuli: Niko tayari kutangulia mbele za haki
- Mpwa wa JPM: Mimi sio Timu Magufuli, Samia ni Timu Magufuli wa kwanza
- Read all related articles