Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpwa wa Magufuli: Kuna wakati mzee nilikuwa nabishana naye

Video Archive
Fri, 6 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa dada wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aitwaye Furaha Dominic amesema miongoni mwa mambo ambayo aliachiwa na kiongozi huyo ni upendo usio na kifani na ari ya kufanya kazi kwa bidi bila kumuonea mtu.

Furaha amesema hayo wakati akifanya mahojiano na Global TV Online katika kipindi maalum cha Hoja kwa Hoja huku akieleza kuwa kiongozi huyo hakuwa mkali kama baadhi ya watu ambavyo wamekuwa wakimtafsiri.

“Hayati Magufuli alikuwa rafiki sana kwa kila mtu, ukiwa mkweli atakupenda sana, alikuwa mkali kwa watu wanaofanya mchezo katika kazi, wala rushwa na wanaokiuka sharia za nchi, lakini alikuwa mpole mno kama utamuelewa.

“Mpaka akuamini akupigie simu, akuandikie meseji fahamu kabisa wewe una kitu cha ziada kwake. Huwezi kumfata tu ukamfikia kirahisi hata kama ni mwanafamilia, alikuwa anataka mtu awe na kitu cha ziada, awe na taarifa sahihi ndipo atakusikiliza, mimi nilipata bahati hiyo.

“Kuna wakati nilikuwa nabishana naye namwambia huenda mimi ni bora kuliko wewe, ninataka nisome nipate mafanikio makubwa katika taaluma yangu (ya Kemia), lakini yalikuwa matani tu ya kifamilia, basi tunacheka.

“Mzee (Magufuli) hakupenda kabisa mimi niingie kwenye siasa, hata mimi sikumwambia wakati naingia kwenye siasa kwa sababu watu wangesema ameingia kwenye siasa kwa sababu ya mjomba wake,” amesema Furaha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: