Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpwa wa JPM afunguka kauli ya Zitto ‘’Wanaompenda Magufuli wakazikwe naye’’

Magu Zitto Furaha Mpwa wa JPM afunguka kauli ya Zitto ‘’Wanaompenda Magufuli wakazikwe naye’’

Fri, 6 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa dada wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aitwaye Furaha Dominiki amesema kuwa hashangazwi na kauli ya Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ya kusema kwamba wanaompenda Magufuli wakazikwe naye kwani ni haki yake ya kikatiba kutoa maoni yake.

Furaha amesema hayo wakati akifanya mahojiano na Global TV Online katika kipindi maalum cha Hoja kwa Hoja huku akieleza kuwa jambo hilo limewasaidia kama familia kuishi maisha ya kawaida bila kujali kwamba mzazi wao ni Rais wa nchi.

“Wakati anaingia madarakani, Magufuli alianza kwa kasi kubwa, wapo walimpenda kutokana na kazi zake na wapo waliomchukia. Alipoanza kusemwa na kutukanwa mitandaoni, sisi kama familia tulikuwa tukiumia, lakini baadaye tulizoea tukaona kawaida.

“Magufuli hakuwa malaika, alikuwa binadamu kama wengine hivyo alikuwa na mazuri na mapungufu yake. Juzi nimesikia kuna mtu mmoja amesema wanaompenda Magufuli wakazikwe naye pembeni, mimi nilifurahi sana.

“Wengine wanasema ooh anamtukana, waliokuwa wanamsaidia mbona hamtoki kujibu. Mbunge mmoja lilimuuma sana lile, lakini sisi tukasema haki yake kusema hivyo, kwa sababu Magufuli naye alikuwa binadamu.

“Hata Yesu alikataliwa. Yapo yanasemwa mengi lakini tunaacha kama yalivyo. Hata maandiko yanasema marehemu hazungumziwi sababu ameshapumzika, tunatakiwa tumzungumzie aliyepo sasa ambaye ni Rais Samia.

“Yapo mengi yanazungumzwa na mengi yatazungumzwa Zaidi lakini sisi tunasema hayatuumizi kwa sababu kama Mungu mwenyewe hakupendwa kwa nini Magufuli apendwe na kila mtu,” amesema Furaha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: