Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lowassa kuagwa kesho Karimjee

Lowassa Edward Wasifu Lowassa kuagwa kesho Karimjee

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema baada ya kuwasili msibani nyumbani kwa Marehemu Edward Lowassa na kusaini kitabu cha Maombolezo ametoa ratiba ya mazishi ambapo amesema katika Siku Tano za maombolezo Taifa litaendelea na shughuli za mazishi ya mpendwa wao na mazishi haya ni mazishi ya kitaifaa.

Amesema siku Jumanne, Februari 13, 2024 mwili utatolewa Lugalo kwenda ukumbi wa karimjee ambapo kutokuwepo na Ibada fupi baada ya hapo wananchi wataweza kupata nafasi ya kuaga mwili ambapo zoezi hilo litaenda mpaka saa saba.

Aidha Waziri mkuu Kassimu Majaliwa amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania watanzania kuendelea kuwa wavumilivu na wastahimilivu katika kipindi hiki kigumu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: