Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lowassa alipigania elimu - Dkt. Mpango

Mpango Lowassa N Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.

Tue, 13 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, amesema miongoni mwa vipaumbele alivyopigania aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Hayati Edward Lowassa ni elimu.

Dk Mpango amesema wakati akitoa salam za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa mwanasiasa huyo nguli katika Ukumbi wa Karimjee na kuongeza kuwa nafasi ya Waziri Mkuu, Lowassa alihimiza uhifadhi na utunzaji wa mazingira.

Amesema kwa sababu hiyo iwe ukumbusho wa kutunza mazingira hasa vyanzo vya maji, ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

“Alikuwa kinara wa vipaumbele vitatu vya kitaifa, na kwa hili sitasahau kwenye kikao kimoja alipoulizwa juu ya vipaumbele alisema cha kwanza ni elimu, cha pili ni elimu na cha tatu ni elimu, kwa sababu hiyo alisimamia kwa uhodari utekelezaji wa sera, mikakati na mipango mbalimbali ya elimu,” amesema Dk Mpango.

“Tunapomuaga leo (hayati Edward Lowassa), tujikumbushe wajibu wa kila mmoja wetu kwa nchi yetu na kuyaishi kwa vitendo mambo yote mazuri tunayojifunza kutoka kwenye maisha yake,”amesema Dk Mpango.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: