Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu magonjwa yaliyomuua Lowassa

Lowassapicc Fahamu magonjwa yaliyomuua Lowassa

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: Mwananchi

Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa (70) amefariki Dunia leo tarehe 10 Februari 2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini (JKCI) Dar es Salaam.

Akitangaza kifo hicho kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia televisheni ya Taifa (TBC), Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango amesema Lowassa amefariki leo saa nane mchana.

Amesema Lowassa amefariki katika hospitali hiyo ya JKCI alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa kujikunja utumbo, matatizo ya mapafu na shinikizo la damu.

“Lowassa ameugua kwa muda mrefu, amekuwa akipatiwa matibabu tangu tarehe 14 Januari 2022 katika hospitali ya JKCI na baadae Afrika kusini na kurejea JKCI.

“Rais Samia aanatoa polea kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu mkubwa pia ametangaza siku tano za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa,” amesema Dk. Mpango.

Chanzo: Mwananchi
Related Articles: