RAais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema uzalendo, uwajibikaji, ushirikiano na maslahi ya nchi, ni miongoni mwa vitu alivyojifunza kwa hayati Edward Lowassa wakati wa uhai wake.
Akizungumza wakati wa kuaga mwili Lowassa, viwanja vya Karimjee Dar es Salaam, Dk Mwinyi amesema namna bora ya kuenzi maisha ya Lowassa ni kuishi maono ya uzalendo na uwajibikaji, ili iwe dira ya kujenga umoja na kupiga hatua za maendeleo.
“Msiba wa mpendwa wetu marehemu Lowassa uendelee kutuunganisha kuwa kitu kimoja, natoa pole kwa wanafamilia ndugu, jamaa na marafiki,” amesema.
- Kisa cha Diana Chilolo kufuta namba ya Lowassa
- Tazama hapa msafara wa mwili wa Lowassa ukipelekwa Karimjee
- Shein, Sumaye waeleza uchapakazi wa Lowassa
- Picha: Matukio mbalimbali katika zoezi la kuaga mwili wa Lowassa
- Fredy Lowassa: Asingekuwa Rais Samia, baba asingefika juzi
- Read all related articles