Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#BREAKING:Edward Lowassa afariki Dunia

Edward Lowassa 70 Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa (70) amefariki Dunia saa nane mchana leo February 10,2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu kwa ugonjwa wa kujikunja utumbo, matatizo ya mapafu na shinikizo la damu.

Makamu wa Rais , Dkt. Philip Mpango ametangaza taarifa za kifo cha Lowassa leo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mpango amesema “Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa masikitiko makubwa anatangaza kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Lowassa ambaye amefariki leo February 10,2024 saa nane mchana JKCI alipokuwa anapatiwa matibabu kwa ugonjwa wa kujikunja utumbo, matatizo ya mapafu na shinikizo la damu”

“Hayati Lowassa ameugua kwa muda mrefu na amekuwa akipatiwa matibabu tangu January 24,2022 JKCI, baadaye akapelekwa kwa matibabu zaidi Afrika Kusini na kurejea Tanzania , Mh.Rais Samia anatoa pole kwa Familia Ndugu, Jamaa, Marafiki na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa kwa Taifa letu”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: